Leo, tarehe 16 Juni 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imefanya Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya zamani, na kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri mhe Akida Bahorera kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wataalamu kutoka idara mbalimbali.
Akiwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, Mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa wa Tanga ndugu Hamu Mwakasola (CEA) amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ilipata hati safi 2023/2024, hii ni kutokana na utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa.
" Lengo kuu la kikao hiki ni kuhakikisha kuwa mapendekezo yaliyotolewa na CAG yanapitiwa kwa kina, kujadiliwa na kuwekwa katika utekelezaji ili kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji ndani ya Halmashauri". Alisisitiza.
Viongozi na wajumbe wa Baraza wameonesha nia ya dhati ya kufanyia kazi hoja zilizowasilishwa na kuhakikisha kuwa mapungufu yote yaliyobainishwa yanarekebishwa kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani itaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na rasilimali kwa maslahi ya wananchi wote wa Wilaya ya Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa