Maadhimisho Siku ya Kasa Duniani, Yafanyika Ushongo Kupitia Taasisi ya SeaSense.
Leo, tarehe 17 juni 2025, kijiji cha Ushongo, Wilayani Pangani, yamefanyika maadhimisho ya Siku ya Kasa Duniani yenye kauli mbiu isemayo " Tunza Kasa, Dumisha Afya ya Bahari".
Tukio hili limeandaliwa na Taasisi ya SeaSense chini ya udhamini wa ( EACOP) shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na uhifadhi wa viumbe hai wa baharini, hususan kasa wa baharini.
Sherehe hizo zilifanyika kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwalinda kasa, ambao wako hatarini kutoweka kutokana na uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira, na uharibifu wa mazalia yao.
Akizingumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Kaimu afisa kilimo mifugo na uvuvi ndg Mohamed Mwaushanga amesema kuwa “ Nitumie fursa hii kuipongeza taasisi ya Sea Sense kwa juhudi zake za kuendelea kuwaelimisha wananchi, kuimarisha ufuatiliaji wa kasa, na kuendesha matukio haya ya kijamii ambayo yanahamasisha ushiriki wa kila mmoja wetu hususani vijan, hii inaonyesha umuhimu mkubwa wa kutunza kasa na kudumisha bahari". Alisema.
Taasisi ya SeaSense imeahidi kuendelea kushirikiana na jamii za pwani kuhakikisha kuwa uhamasishaji na uhifadhi wa kasa unakuwa endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa