Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, ameonesha kuvutiwa na ubunifu wa bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wadogo wadogo alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki leo tarehe 2 Agosti 2025, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane mkoani Morogoro.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Pinda amewapongeza wajasiriamali kwa juhudi zao katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, akibainisha kuwa jitihada hizo ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Bidhaa hizi mnazozalisha ni ushahidi kuwa wajasiriamali wetu wanajituma. Na ni muhimu sasa kuongeza kasi na ubunifu zaidi ili kuleta ushindani ndani na nje ya nchi,” alisema Mhe. Pinda.
Aidha, amezitaka Halmashauri na taasisi za kifedha kushirikiana kwa karibu na wajasiriamali kwa kuwawezesha kupata mafunzo, masoko na mitaji ili kukuza biashara zao.
Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi” na yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 8 Agosti 2025.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa