Prof. Shemdoe afika Mwera na Kimang’a kukagua miundombinu ya Elimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe amekagua ujenzi wa shule shikizi ya msingi ya Mwera pamoja ujenzi wa shule mpya ya bweni ya sekondari Kimang'a zilizopo wilayani Pangani Mkoani Tanga.
Prof. Shemdoe amefanya ukaguzi huo wakati wa ziara yake Wilayani humo mapema tarehe 16.11.2021z
Akikagua shule hizo Prof. Shemdoe ameonyeshwa kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa Shule hizo hasa shule mpya ya sekondari ya bweni ya Kimang'a ambapo amefurahishwa na muda mchache waliotumia katika ujenzi huo huku akiwataka viongozi wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha shule hizo zinakamilika kabla ya disemba 15, 2021 kwa ajili ya wanafunzi kuanza masomo ifikapo Januari,2021.
"Nitoe msisitizo madarasa haya ifikapo tarehe 15 disemba 2021 vile vyumba vya madarasa viwe vimekamilika, tukabidhiwe ili kujiandaa sasa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi Januari". Prof.Riziki Shemdoe Katibu Mkuu
Pia Prof. Shemdoe amewataka kuangalia namna ya kubadilisha aina ya ujenzi kwa kutumia mapaa mawili badala ya manne ili kupunguza gharama za ujenzi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa