Leo tarehe 16 Septemba 2025, Wakuu wa Idara na Vitengo,Wakuu wa Shule, Waganga wafawidhi,Matabibu pamoja na Watendaji kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wamepata Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kupitia mfumo wa kidijitali wa GAMIS.

Mafunzo haya yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya zamani, Pangani, yakiwa na lengo la kuongeza ufanisi, uwajibikaji na udhibiti thabiti wa mali za umma.
Akiwasilisha mafunzo hayo ndg Martin Kauzen afisa usimamizi wa mali za Serikali Mkoa wa Tanga amesema kuwa
"Mfumo wa usimamizi wa mali za Serikali ni lazima kwa kila taasisi na mfumo huu una manufaa makubwa ikiwemo kujua kiwango cha mali kilichopo kwenye Nchi kwa ujumla". Alisema.
Aliongeza kuwa Kupitia mfumo wa GAMIS, viongozi na watendaji watakuwa na uwezo bora zaidi wa kusimamia rasilimali za wananchi kwa uwazi na uadilifu, hatua inayoongeza imani ya jamii kwa Serikali yao.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa