Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya mahitaji ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2024 kwa Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Micap Village Kilichopo kata ya Bweni Wilayani Pangani.
Akizungumza leo Disemba 30,2023 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani, wakati wa kukabidhi mahitaji hayo (Mkono wa heri ya Mwaka Mpya kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan), Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Ndg. Ester Gama amesema jambo hili ni juhudi za Serikali za kuboresha ustawi wa jamii hususan katika kulea na kutunza watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu.
"Kwa namna ya pekee naomba mpokee salamu za Serikali, zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae anatambua kazi kubwa mnayoifanya katika kulea Watoto na leo imempendeza Rais wetu kutupatia zawadi hii kwa ajili ya kufurahi pamoja katika kipindi cha Sikukuu hii ya mwaka mpya 2024”.
Msaada uliotolewa ni pamoja na Mchele, Sukari, Unga, Sabuni, Mafuta ya kupikia, Mbuzi na zawadi nyingine za kuwapa Watoto faraja.
Akizungumza mala baada ya kupokea msaada huo Msimamizi wa kituo Bi. Anna amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais mpenda watu Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kuwakumbuka watoto hawa na kuwapa tabasamu na furaha katika kipindi hiki cha kusherehekea Siku Kuu ya mwaka mpya 2024.
"Mungu awabariki sana, tunawashukuru kwa msaada huu tumeupokea na watoto wamefurahi sana”
Ameendelea kutoa wito kwa jamii kuzidi kuwakumbuka na kuwatembelea kwani watoto hao ni sehemu ya jamii ya Watanzania.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa