Leo tarehe 17 Septemba 2025, wananchi wa Kipumbwi, Wilayani Pangani, wamejumuika kushuhudia hafla ya makabidhiano ya eneo la mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Samaki kwa mkandarasi rasmi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Burian, pamoja na Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani, Mhe. Jumaa Aweso. Pia walikuwapo Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Isaya Msuya, na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Wananchi wameishukuru Serikali kwa juhudi zake kubwa za maendeleo ya kiuchumi, kuongeza ajira, na kuboresha masoko ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa pwani ya Pangani.

Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa