Chalamila Avutiwa na Maziwa Kutoka Pangani _Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, leo tarehe 6 Agosti 2025, ametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Chalamila alivutiwa na bidhaa za maziwa zinazozalishwa Pangani kutoka kwa wafugaji wadogo wa Mkoa wa Tanga, akisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani katika mazao ya mifugo ili kuchochea uchumi wa wananchi vijijini.
Alipongeza juhudi za Halmashauri ya Pangani kwa kuhamasisha ujasiriamali kupitia sekta ya mifugo, hasa uzalishaji wa maziwa bora, na kuwataka wananchi kuendelea kutumia fursa ya maonesho kujifunza mbinu bora za ufugaji na usindikaji wa maziwa.
Maonesho ya Nane Nane yanaendelea hadi tarehe 8 Agosti, yakibeba kauli mbiu: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa