Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Waziri Kindamba akiongozana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi. Pili H. Mnyema na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tanga. Leo tarehe 27/05/2023 amefanya Ziara Katika Wilaya ya Pangani. Amepokelewa na Mkuu wa wilaya ya Pangani, Mh. Zainab Abdallah Issa, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Pangani, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Pangani na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Isaya M. Mbenje.
Katika ziara hiyo Mh. Mkuu wa Mkoa alitembelea na Kukagua Miradi yote ambayo itapitiwa na Mwenge wa Uhuru tarehe 10/06/2023 katika Wilaya ya Pangani. Mh. Mkuu wa Mkoa alianza na kukagua Mradi wa Ukarabati wa Soko la Pangani Mjini. Na baadae alielekea kukagua Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi katika Zahanati ya Ushongo, Ujenzi wa Ofisi ya Udhibiti Ubora Wilaya ya Pangani, Ujenzi wa jengo la UZIKWASA, Ujenzi wa Barabara ya Malapa iliyopo Pangani Mjini , Mradi wa Maji Sakura ,Shughuri za Mazingira ambazo zinatekelezwa na BMU na mwisho Mradi wa Kikundi cha Vijana JIFUTE.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa