Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Balozi Dkt. Batilda Burian,( kulia) amekabidhi gari pamoja na Pikipiki mbili kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya zitakazo tumiwa na mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ( RUWASA).
Balozi Batilda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya maji, hatua inayoonesha jitihada za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa Maji safi Vijijini.
Hafla hiyo imefanyika leo Novemba 1, 2024, mkoani Tanga.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa