Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SEA SENSE imebainisha umuhimu wa kudumisha matumizi endelevu ya rasilimali za baharini kwa kusaidiana na wanajamii katika kuhifadhi rasilimali hizo kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo.
Hayo yamefanyika leo Agosti 22,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi bwa Abdalla Ngaugula msimamizi mkuu wa mradi amebainisha kuwa Wilaya ya Pangani ilipata nafasi ya kutekeleza mradi wenye kujenga uwezo wa wananawake katika jamii za wavuvi za pwani ya Tanzania kushiriki kikamilifu katika kusimamia na kutunza rasilimali za bahari.
" Katika Wilaya yetu ya Pangani mradi huu ulitekelezwa kwenye vijiji vinne ambavyo ni Choba, Ushongo, Kipumbwi na Sange". Alisema
Ameongeza kuwa endapo bahari haitatunzwa vizuri basi kutakuwa na madhara ya kiikolojia, athari za kiuchumi, kupungua usalama wa chakula, uharibifu wa bioanuai, mabadiriko ya tabia nchi.
Aidha mradi huu umefanikiwa kwa kuongezeka kwa uelewa ulioimarishwa wa mifumo ya Mazingira ya Baharini , uboreshaji wa maisha, pamoja na uhifadhi wa kasa na nguva.
Taasisi ya Sea Sense imejikita katika kubainisha mpango mkakati unaolenga maeneo muhimu ikiwemo tafiti na uhifadhi, elimu, mafunzo,kujenga uwezo kwa jamii za pwani kuwa na maisha endelevu pamoja na utawala bora.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa