Leo, tarehe 18 juni 2025, taasisi ya SeaSense chini ya udhamini wa ( EACOP) shirika linalojihusisha na uhifadhi wa viumbe hai wa baharini, hususani kasa limekabidhi vifaa vya doria kwa kamati za usimamizi wa mazingira ya Pwani (BMU wa wilaya ya Pangani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ulinzi wa rasilimali za baharini na kuhamasisha uvuvi endelevu.
Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa vya kujiokolea pamoja na elimu ya kuvitumia, Tochi ya kuchaji kwaajili ya doria ya usiku, Makoti ya Mvua 5, kwaajili ya usalama.
Mtaalamu wa utafiti kutoka taasisi ya Sea Sense ndugu Omari Abdallah alieleza kuwa msaada huu unalenga kuiwezesha kamati za usimamizi wa mazingira ya pwani kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa maeneo ya bahari na viumbe kama kasa, nguva, na samaki walioko hatarini kutoweka.
" Kila mmoja anapaswa kuzingatia usalama wake binafsi wakati wa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kujifunza kuogelea pamoja na kuwa na taarifa sahihi ili kurahisisha majukumu yao ya kila siku". Alisema.
Aidha aliongeza kuwa wavuvi wote wanapaswa kuwa na leseni ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa njia halali.
Mmoja wa wavuvi walionufaika alisema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuzuia uvuvi haramu na pia kuongeza usalama wao wakati wa shughuli zao za uvuvi na doria.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa