Walimu wapya waliopata ajira katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wamepatiwa semina elekezi leo, tarehe 10 Julai 2025.
Semina hiyo iliyoendeshwa na Tume ya utumishi wa walimu (TSC) Wilaya ya Pangani, imefanyika katika ukumbi wa TRC ikiwa na lengo la kuwajengea uelewa kuhusu taratibu za kazi, maadili ya utumishi wa umma pamoja na majukumu yao katika sekta ya elimu.
Viongozi kutoka idara ya elimu na utumishi walitoa maelezo ya kina, wakisisitiza umuhimu wa nidhamu, uwajibikaji na ubunifu katika kufundisha.
Semina hiyo ni hatua muhimu ya kuwaandaa walimu hao wapya ili kuanza kazi zao kwa mafanikio na kwa kuzingatia maadili ya kazi ya ualimu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa