Leo, tarehe 23 Septemba 2025, watumishi wa afya ngazi ya jamii, watendaji kata na viongozi wa dini wamekutana katika semina maalum ya Uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti, iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego kwa udhamini wa Pfizer Foundation katika ukumbi wa hospitali ya Wilaya ya Pangani.
Lengo kuu la semina hiyo ni kuimarisha uelewa kuhusu uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti na kuhamasisha jamii kuchukua hatua za kulinda afya ya mama, dada na binti zetu.
Akiwasilisha lengo la mradi huo wa uchunguzi wa Saratani ya Matiti Dkt. Sunday Wanyika kutoka taaisi ya Jhpiego ameeleza kuwa mradi huu unalengo la Kuongeza vituo vinavyotoa huduma za uchunguzi wa awali, Kuwafikia wananchi kwa karibu kupitia viongozi wa jamii pamoja na Kutoa elimu ya kujichunguza na kugundua dalili mapema.
Alisema kuwa " Kwa kushirikiana na viongozi wa jamii, tunaleta elimu na huduma karibu na wananchi ili kila mmoja apate taarifa sahihi na msaada unaohitajika".
Kumbuka: Uchunguzi wa mapema unaokoa maisha.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa