Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Climate Action Network Tanzania (CAN) imetoa elimu ya ufugaji bora wa Nyuki na uhifadhi wa mazingira (mikoko) pamoja na maendeleo ya mradi kijiji cha Msaraza na kigurusimba.
Hayo yamefanyika leo Agosti 27, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akiwasilisha taarifa ya mradi uliopo kijiji cha Msaraza Bi Miriamlisa amesema tunatarajia kutoa elimu ya uhifadhi katika maeneo ya Msaraza na Kigurusimba na kugawa mizinga ya kufugia nyuki.
"ni muhimu sana jamii itambue umuhimu wa ufugaji wa nyuki, kwani nyuki wanafaida sana katika kutunza mazingira, kupata nta pamoja na asali , hivyo ni wakati sahihi kwa jamii kuwekeza katika ufugaji wa nyuki. Alisema.
Aidha kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira ndg Twahiru Mkongo amepongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za uhifadhi wa mazingira.
" tukitoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira na wakawekeza katika mizinga ya nyuki basi tutakuwa tumehifadhi misitu yetu na kuongeza pato katika jamii". Alisema.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa