Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga, (UWASA) wamekabidhi mradi wa ujenzi wa Vyoo vya kisasa Matundu 8 katika Shule ya Msingi Funguni.
UWASA wamekabidhi mradi huo 21 julai 2023, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Abdallah akiwa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakati wa ziara ya twende na Samia kijiji kwa kijiji.
Akisoma taarifaya ya ujenzi wa mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly amesema "mamlaka itatoa hamasa na elimu kwa wananchi ili kujenga vyoo vitakavyo endana na usafi wa mazingira kama walivyovijenga katika shule hiyo,na tayari Mradi wa Ujenzi wa Vyoo Matundu (8) katika Shule ya Msingi ya Funguni umekamilika kwa asilimia 100%, hivyo unaweza kuanza kutumika rasmi kuanzia sasa ili kusaidia wanafunzi wa Shule hio kuwa na mazingira salama".
Mradi wa ujenzi wa matundu 8 ya vyoo kwa shule ya msingi funguni umekuja baada ya uwepo wa utekelezaji mradi wa ujenzi wa mfumo wa kupokea na kutibu maji taka unaotekelezwa kwa lengo la kuboresha huduma ya uondoshaji wa maji taka taka kwa jamii ya wakazi wa pangani mjini.
#panganimpya#
#twendenasamia
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa