Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), leo tarehe 13, Machi 2024, limetambulisha Mradi wa Suluhisho la Ujumuishwaji wa Misitu na Nishati Tanzania, Wilayani Pangani.
Hayo yamefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na kuhudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya Bi Ester Gama, Mwenyekiti wa Halmashauri Akida Bahorera,Makamu Mwenyekiti mhe Zainab Mvaa,Katibu wa CCM Wilaya ya Pangangi Bw Abdul Swala, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa idara na Vitengo pamoja na Waheshimiwa Madiwani.
Akifungua kikao hicho Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Bi Ester Gama amelipongeza Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania kwa kutoa Elimu na kuhimiza kuwa utunzaji wa misitu uwe endelevu kwa wananchi ili kuendelea kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania.
Akiwasilisha Taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TFCG ndg Charles Meshack amesema kuwa mradi huu ni wa miaka mitatu (3), na unafaida nyingi kwenye vijiji ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake meneja wa mradi Ndg Saimon amesema kuwa lengo kuu ni kuimarisha usimamizi endelevu wa mazingira na misitu, na mradi huu unatarajiwa kufanyika katika vijiji vitatu hapa Pangani ambavyo ni Mseko,Mtango na Kwakibuyu.
Bw. Saimon amesisitiza kuwa mradi huu utalenga kutoa elimu kwa maafisa misitu na Wataalam kuhusu usimamizi wa Misitu ya jamii,utawala bora na uvunaji endelevu wa Misitu.
Waheshimiwa Madiwani walipata nafasi ya kutoa maoni mbalimbali kuhusu mradi huo ambapo wameupokea mradi huo na kupongeza kwa elimu iliyotolewa yenye lengo la kuwainua Wananchi kiuchumi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa