Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah ameanza ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa shughuli za kiserikali alioipa jina la twende Nasamia.
Ziara hio imeanza rasmi leo tarehe 10.07.2023 katika shule ya msingi Pangani, akiungana na Kamati ya Usalama ya Wilaya,viongozi wa Chama cha Mapinduzi,Waheshimiwa Madiwani,Ofisi ya Mbunge,Wakuu wa taasisi pamoja na watendaji na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa.
Ziara hiyo itahusisha kutembelea vijiji vyote vya wilaya ya Pangani na kukagua miradi yote ya maendeleo na kushiriki mikutano na wananchi yenye lengo la kutatua changamoto za wananchi.
Aidha Mhe. Zainab Abdallah ametoa wito kwa wasimamizi wa Miradi hio kukamilisha kwa haraka shughuri hizo na kusema" hakikisheni mnafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mAAiradi hio haraka ili ianze kutumika".
#panganimpya
#Twendenamama
#Kaziiendelee
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa