Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Julai 28,2023, limefanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti.
Madiwani hao wamepiga kura na kumchagua Mh Zainabu Mvaa Msagati kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa muhula wa Pili.
Mwenyekiti wa Halmashauri akisoma matokeo ya uchaguzi huo amesema kuwa "Jumla ya kura zote zilizopigwa 19 kura zilizoharibika ni O, kura za hapana ni 0, kura za ndio 19, hivyo Makamu Mwenyekiti ameshinda kwa kura zote 19.
Mala baada ya kuchaguliwa Mhe Zainabu Mvaa amesema kuwa anawashukuru Madiwani wote kwa kumpigia kura na kumheshimisha na ameahidi kuendelea kuwatumikia wanapangani kwa weledi.
Hata hivyo mwenyekiti wa Halmashauli ya Pangani Mheshimiwa AKIDA OMARI BAHORERA amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwan. ISAYA M MBENJE kwa ushirikiano mkubwa pamoja na Wakuu wa idara na Vitengo. Vilevile amevunja kamati za awali na kuwapongeza lakini pia ameunda Kamati mpya zilizochaguliwa , kamati zilioundwa ni kamati ya Elimu Afya, Kamati ya Uchumi, Kamati ya Maadili,Kamati ya Ukimwi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa