Shule ya msingi Kigurusimba ni moja kati ya Shule 3 zilizopo kata ya Masaika, Wilayani Pangani yenye jumla ya Wanafunzi 351 kati ya hao wanafunzi wa kiume ni 171 na wanafunzi wa kike ni 180
Taarifa ya Mradi wa shule hio imesomwa Julai 20, 2023 mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Abdallah, akiwa katika ziara ya Twende na Samia kijiji kwa kijiji yenye lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali na kusema kuwa " Tunaishukuru Serikali kwa kutuwezesha kupata fedha kiasi cha shilingi milioni 20, kutoka Serikali kuu kwaaajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa, sote tumekuwa mashahidi mradi huu umekamilika na unavutia sana".
Kwa upande wake mwenyekiti kamati ya ujenzi Mashaka Hamisi Abdallah amesema kuwa " Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa jimbo la Pangani Juma Aweso pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya pangani bwana Isaya M Mbenje kwa jitihada zao za kusimamia shughuli zote za uboreshaji mazingira na miundombinu ya kujifunzia kwa wanafunzi wetu.
#twendenasamia
#kijijikwakijiji
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa