Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah , Julai 12, 2023, amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili katika shule ya msingi mkalamo kupitia fedha za Mradi wa Uboreshaji upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania (BOOST).
Akiwa katika eneo la mradi huo wa ujenzi, Mhe. Zainabu ameipongeza kamati ya ujenzi na uongozi wa halmashauri ya Pangani na kusema kuwa "kazi nzuri imefanyika lakini nawaagiza wasimamizi wa miradi, na Mafundi kuhakikisha kazi za ujenzi zinakamilika na kukabidhiwa kwa wakati uliotolewa".
Ameongeza kuwa Mafundi wanapaswa kuendelea kufanya kazi usiku na mchana ili kuwawezesha watoto kuendelea kusoma katika mazingira mazuri, "haiwezekani watoto kuendelea kusoma katika mazingira ya msongamano wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameleta fedha za kutosha kujenga vyumba vya madarasa".
Ujenzi wa vyumba hivi viwili vya madarasa kupitia mradi huu wa BOOST, Umegharimu takribani Shilingi milioni 56, zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
#panganimpya
#kijijikwakijiji
#twende na Samia
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa