Pangani_Tanga.
Serikali ya awamu ya Sita chini ya rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuipa thamani sekta ya afya kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
Wilaya ya Pangani ni miongoni mwa Wilaya zilizopokea Milioni Mia tisa( 900m), fedha kutoka Serikali Kuu kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya.
Kupitia Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya, imeendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya hospitali ya Wilaya.
Hatua za ukarabati kwa awamu ya kwanza wa Majengo ya RCH, upasuaji, Jengo la kuhifadhia maiti na wodi namba 2 tayari yamekamilika.
Hata hivyo, ukarabati upo katika awamu ya pili kwa majengo ya wodi 1 na 3 ambayo yapo katika hatua za upauaji. Pia ukamilishaji wa jengo la OPD unaendelea hatua za kupaka rangi.
Hadi sasa kiasi cha shilingi Milioni 347,473,223, zimetumika katika utekelezaji wa ukarabati huu wa hospitali kongwe ya Wilaya ya Pangani.
#pangani mpya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa