Usafi wafanyika maadhimisho ya Mashujaa.
Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Pangani leo Julai 25,2024 wameadhimisha siku ya mashujaa kwa kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo ya feri pamoja na sokoni.
Ikumbukwe kuwa kila ifikiapo Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania.
Siku hii pia huambatana na Shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalumu za kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea Amani ya Nchi kutoka kwa Viongozi wa Dini.
Kwa kuunga mkono jitihada hizo wananchi wa Wilaya ya Pangani wamejitokeza kushirikinusafi wa mazingira na upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku hiyo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa