VIKUNDI 29 VYAPEWA MIKOPO YA ASILIMIA 10% PANGANI
Pangani _ Tanga.
Leo tarehe 3 Disemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya amezindua rasmi zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10%.
Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Pangani, ambapo jumla ya vikundi 29 vya vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu, vimepatiwa Mkopo wenye thamani ya Shilingi milioni 254, inayotengwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza mala baada ya Uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Pangani, mhe Gift Isaya Msuya amesema kuwa vikundi vyote vilivyopewa mikopo vifanye kazi iliyokusudiwa ili viweze kunufaika na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati, ili kundi lingine liweze kunufaika na mikopo hii.
" Serikali imeamua kurejesha mikopo hii ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu, ikiwa na dhamira ya kutoa ajira na kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa Mkoa wetu kwa ujumla". Alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha Boda Boda bwa Alhaji Omary amesema tunapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuyakumbuka makundi yote na kuyawewezesha kupata mikopo hii kwa awamu nyingine toka isitishwe.
"sisi kama wana kikundi tutautumia vizuri mkopo huu na kuhakikisha tunarejesha kwa wakati ili wanufaika wengine wapate fursa hii". Alisema.
Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,Mwenyekiti wa Halmashauri, Viongozi wa vyama vya siasa, katibu wa Mbunge, diwani wa viti maalumu,Viongozi wa taasisi za fedha pamoja na wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa