Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Juvenal Nkonoki amevihimiza vikundi vya Wavuvi na Wachakataji Dagaa vya Wilayani Pangani Mkoani Tanga kudumisha umoja na ushirikiano kwani huo ndiyo mtaji wa maendeleo.
Prof. Nkonoki ameyasema hayo Jumatatu September 18, 2023 katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya siku mbili ya kuvijengea uwezo vyama vya ushirika kwa vikundi 11 vya Wavuvi na Wachakata Dagaa vyenye jumla ya wanachama 218 ambapo kati yao Wanawake 118 na Wanaume 100. Mafunzo hayo yamefanyika katika Kijiji cha Sakura Kata ya Kipumbwi Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.
“Mkiwa katika umoja tunaimani hata tukiwajengea uwezo mtakuwa na nguvu ya kutoka pale mlipo na kwenda sehemu nyingine kwa vile mtakuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya uvuvi. Tunaamini kwa umoja wenu mafunzo haya yanakwenda kuwa chachu ya mabadiliko kwenu na mnao wawakilisha”
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa