Wadau wa Sekta Mtambuka katika utekelezaji wa Afua za Lishe, wamekutana na kufanya kikao cha awali na kujadili mpango wa Bajeti ya Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Kikao hicho kimefanyika Novemba 28,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na kuhudhuliwa na Afisa Lishe mkoa wa Tanga Bi Sakina Mustafa, Maafisa Lishe wa Wilaya ya Pangani pamoja na Wadau wa sekta Mtambuka ya Utekelezaji wa Afua za Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akiongea mala baada ya ufunguzi wa kikao hicho ,Bi Sakina Mustafa amesema kuwa lengo la kikao ni pamoja na kujadili bajeti ya utekelezaji wa Afua za Lishe kwa kuzingatia Vipaombele vya mpango jumuishi na kuwaomba maafisa Lishe na wadau kupanga bajeti ya Lishe kulingana na Vyanzo vya Fedha vilivyopo katika Halmashauri, ili kurahisisha shughuli za Lishe na kuweza kuleta matokeo chanya katika jamii.
Aidha amesisitiza kuwa agenda ya Lishe ni jukumu la kila mmoja katika jamii na kuitaka jamii kuipa nafasi ili kuweza kupata jamii yenye afya bora.
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Pangani Daud Mwakabanje ameendelea kutoa wito kwa jamii kuendelea kushikaman na kujitokeza hasa pale panapokuwa na maadhimisho mbalimbali ya Lishe ili waweze kupata elimu bora ya Lishe.
Bi Sakina amesisitiza kuwa Bajeti ya Lishe izingatie mpango jumuishi ili kupata bajeti inayotekelezeka hasa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
#panganimpya
#lishekwajamiibora.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa