Septemba 13,2023, Wataalamu kutoka kata ya Madanga, ikiongozwa na Afisa Mifugo wa kata bwan Joe Mapunda, wamekutana na Wafugaji, na kuwapa Elimu ya chanjo ya Mifugo yao ikiwemo Ng'ombe, na Mbuzi.
Tukio hilo limehudhuriwa na wafugaji, Mtendaji wa kata ya Madanga bwan Rajab Shame, Mtendaji wa Jaira bwan Mtanzania Wasaa pamoja na Mtendaji wa Madanga bi Fatuma Muhaka, ambapo, wafugaji wameelezwa kuwa ni muhimu kuzingatia sheria ili kuepuka migogoro mbalimbali, na kuhimizwa juu ya umuhimu wa chanjo.
"Faida za Chanjo kwa Mifugo ni pamoja na kukinga wanyama dhidi ya Ugonjwa wa Mapafu , hivyo kuchanja kutapunguza Vifo kwa mifugo na kupata Mifugo bora kwa matumizi na kuongeza pato kwa jamii hasa zinazojihusisha na ufugaji".
Kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Bwan Joseph ameongeza kuwa Chanjo kwa mifugo ni muhimu ili mifugo iwe salama na bora zaidi kwa matumizi, hivyo jamii ya Wafugaji wachanje Mifugo yao bila kukosa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa