Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa NeST na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma, katika ngazi za chini za Serikali za Mitaa.
Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 19 Machi 2025 katika Ukumbi wa YMCA, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Watumishi hao ili waweze kufanya Manunuzi ya vifaa mbalimbali kwa urahisi.
Akiongea na washiriki wa mafunzo hayo, mwezeshaji wa mafunzo kutoka PPRA amesema kuwa "Mfumo huu wa NeST ni rafiki na rahisi kwa watumiaji, ni mfumo wa wawazi na shirikishi hivyo unaondoa mianya yote ya upendeleo, udanganyifu na rushwa na utaongeza uwajibikaji na uwazi katika kufanya ununuzi ya Umma".
Ameongeza kuwa ununuzi wa umma unajumuisha kutambua na kuandaa mahitaji,uchaguzi na mwaliko wa zabuni, maandalizi ya mkataba tuzo na usimamizi wa mikataba. Alifafanua.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Manunuzi na Ugavi ndugu. Mawazo Mbunda alisema kuwa "Mfumo huu ni rafiki sana kwani unatupatia wasaa wa kutimiza majukumu yetu mama, kwasababu kabla ya mfumo huu kulikuwa na mzunguuko mrefu wa kufanya manunuziā. Alisema.
Mfumo mpya wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya kielektroniki (National e-procurement system of Tanzania_NEST) ambao ulianza kutumika rasmi tarehe mosi Oktoba, 2023 baada ya mfumo wa zamani wa TANePS kufika ukomo wake.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa