Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Mussa Kilakala, ameongoza zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee kwa lengo la kutambulika na kupata huduma ya Afya bure katika hospitali za Serikali.
Zoezi hilo limefanyika leo Julai 1, 2024 katika Zahanati ya Kigurusimba iliyopo kata ya Masaika ambapo makabidhiano hayo yamefanyika.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa Vitambulisho hivyo, Mhe. Mussa Kilakala, amewahakikishia wazee hao kuwa zoezi hili ni endelevu kwa Kata zote 14 ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Wilaya ya Pangani anapata kitambulisho hicho na kuweza kupatiwa matibabu bila malipo.
"Kipekee tuendelee kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini wazee, ambao mmetumia nguvu nyingi kulihudumia taifa, mmejenga jamii nzuri hapa Pangani, mhe Rais ameona ipo haja kwa kazi kubwa mlofanya ya kutoa msamaha maalumu ya kuwapa vitambulisho kwaajili ya matibabu".
Sambamba na hilo mhe Mussa Kilakala, amewaelekeza wataalamu wa afya chini ya Mganga Mkuu, kuhakikisha kuwa vitambulisho hivyo visiwe adha kwa wazee hao na badala yake wapatiwe huduma kwa haraka pindi watakapo hudhuria kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya ndani ya Wilaya ya Pangani.
Aidha kwa upande wake Afisa Ustawi ndg , Abeid Hamisi amewataka wazee wote waliopata vitambulisho vya msamaha wa matibabu kuanza matibabu katika ngazi ya Zahanati.
" Idadi ya vitambulisho vilivyo tayari kugawiwa ni jumla ya 2250 sawa na asilimia 41 ya wazee wote waliojuu ya umri wa miaka 50". Alisema
#afyanimtaji
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa