Akionyesha hisia zake za furaha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NIACHE NISOME PANGANI INANITEGEMEA, Agosti 19,2023, Prof. Adolf Mkenda amesema ni wakati sahihi kwa maeneo mengine kwa ujumla kuja Pangani kuendelea kujifunza zaidi juu ya masuala ya Elimu.
"Elimu ni Ufunguo wa maisha kwahio
ukimnyima Mtoto Elimu, Ume
mnyima Maisha, kwani mafanikio ya waliosoma ni chachu ya wengine kuongeza bidii kwenye kusoma".
Pangani mmefanya jambo zuri sana la kuigwa na maeneo mengine ili kuendeleza na kukuza Elimu, Tanzania, na kiukweli nimeona kazi nzuri sana na naomba tuendelee kushikamana.
Hata hivyo Waziri ameongeza kuwa ombi la ufunguzi wa chuo cha Veta kilichopo Wilayani Pangani rasmi kitaanza kufanya kazi mwezi wa tisa (9 ) mwaka huu na hii itajumuisha Vyuo vyote vya Veta
vilivyopo Mkoani Tanga kuanza kufanya kazi.
Prof. Adolf Mkenda ameongeza kuwa kutokana na maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Tanga rasmi sasa unaenda kupata kampasi ya chuo kikuu cha Mzumbe, na hii itarahisisha Wanafunzi wetu kupata Elimu yao ya Chuo kikuu hapa hapa Mkoani Tanga.
#niachenisome#panganimpya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa