Waziri wa TAMISEMI, Mohamedi Mchengerwa leo August 15,2024 amewatangazia Watanzania na Vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa November 27, 2024 itakuwa ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara.
Mchengerwa amesema upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni ambapo kwa mujibu wa kanuni kampeni za uchaguzi zitafanyika siku saba kabla ya siku ya uchaguzi “Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni”
“Ninawatakia uchaguzi mwema, amani na utulivu katika kipindi chote cha uandikishaji, uteuzi wa Wagombea, kampeni, upigaji kura, wakati wa kutangaza na kupokea matokeo ya uchaguzi, kwa tangazo hili Wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura, kugombea na kushiriki katika Uchaguzi huu ili kupata viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo ya Nchi yetu”
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa