Waziri wa Ujenzi Mhe Innocent Bashungwa amefanya ziara na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Barabara , Tanga_Pangani_Saadani_Bagamoyo na ujenzi wa Daraja la mto Pangani.
Ziara hio imefanyika leo Novemba 23,2023 Wilayani Pangani.
Waziri Bashungwa amemhimiza mkandarasi kuhakikisha mradi wa ujenzi wa daraja unakamilika kwa wakati na ubora ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe Bashungwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Pangani ambae pia ni Waziri wa Maji mhe Juma Aweso, na Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah pamoja na Kamati ya siasa ya Wilaya ya Pangani.
Ikumbukwe kuwa Mhe Aweso anaendelea na Ziara katika kata mbalimbali zilizopo Wilayani Pangani na lengo ni kutatua kero kwa Wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa