Katika kuhakikisha utekelezaji wa afua za lishe unazingatia malengo ya kitaifa, Wilaya ya Pangani imefanya kikao cha tathmini ya robo ya tatu ya mkataba wa lishe, kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mhe. Gift Isaya Msuya.
Kikao hicho kimefanyika leo Mei 19, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Zamani kimekusudia kutathmini utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha jamii inanufaika na huduma bora za lishe.
Akizungumza katika kikao hicho mhe Gift Isaya Msuya amewataka watendaji kuendelea kusimamia kwa karibu kila kata ili kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele katika jamii zetu.
Aidha, Mratibu wa Lishe wa Wilaya ndg Daud Mwakabanje ametoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe ikiwemo utoaji wa elimu na unasihi wa lishe ambapo jumla ya wateja 482 waliohudhuria kliniki ya baba mama na mtoto kwaajili ya kupata huduma za afya ya uzazi katika vituo vya kutolea huduma za afya, usambazaji wa mashine ya kuchanganyia madini joto kwenye chumvi, na kutoa unasihi wa ulaji unaofaa kwa wagonjwa wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi na waliogundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari. Alisema.
Alibainisha kuwa changamoto za mwitikio mdogo wa Wanaume kushiriki kwenye Siku ya Afya na Lishe jambo linalopelekea wanaume kukosa uelewa wa kutosha juu ya elimu sahihi ya afya na lishe kwa kaya zao, hivyo kwa kushirikiana na Watendaji wa kata na Vijiji kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia mikutano kuhusu umuhimu wa Wanaume kuhudhuria.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa