Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Malipo. Pia, kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 wanafunzi wa kidato cha Tano na sita hawatalipa ada. Lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata nafasi hiyo na kukamilisha mzunguko wa Elimu ya Msingi na Sekondari bila vikwazo
Pamoja na mafanikio haya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imebaini kuwa, uendeshaji wa elimu una changamoto ambazo hazina budi kutatuliwa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu. Kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimumsingi na pia changamoto za uboreshaji wa Elimumsingi na Sekondari, nini Kifanyike.
Mkakati huu umebainisha changamoto mbalimbali zinazoathiri ufanisi na mafanikio katika elimu. Aidha , mkakati umechambua kwa undani hali halisi ilivyo na kuonesha fursa zilizopo, utatuzi wa changamoto pamoja na viashiria vya upimaji wa mafanikio ya utekelezaji wa mkakati huo.
Mkakati huu ni zana muhimu itakayoisaidia Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuwa na wahitimu wenye umahiri uliokusudiwa
Uzinduzi wa mkakati ulifanyika kitaifa Mkoani Tabora na Baadae kufanyika ki mkoa, Wilaya, Halmashauri,Tarafa, Kata, Mtaa/kijiji na kila shule. Hivyo Kila kiongozi ataweka utaratibu unaoendana na mazingira ya eneo lake ili kuhakikisha kua mkakati huu unatekelezwa na kuleta matokeo tarajiwa. Kila mdau anayehusika na utekelezaji wa mkakati huu autumie kama kioo cha kujipima ni kwa namna gani wajibu na majukumu yake
Ili kutekeleza hilo, Wilaya ya Pangani imefanya uzinduzi wa mkakati ki Wilaya, uzinduzi huo umefanyika Leo tarehe 16/09/2022 saa 8:00 asubuhi katika Ukumbi wa Seaside. Uzinduzi huo ulihudhuliwa na Mwanyekiti wa Uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mh.Ghaibu Lingo pia Uzinduzi huo ulihudhuliwa na DAS wa Wilaya ya Pangani, Hassani Nyange, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Lucy Gurtu ambaye ni Afisa elimu sekondari Wilaya ya Pangani, Kaimu Afisa elimu Sekondari na pia Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw Leonard Komba, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi Wilaya ya Pangani, katika uzinduzi huo pia walikuwepo Wah. Madiwani wote wa Kata mbalimbali za Wilaya ya Pangani, Wakuu mbalimbali wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Maafisa Elimu Kata wa kata zote za Wilaya ya Pangani, Viongozi mbalimbali wa Dini, Wadau mbalimbali wa Elimu na Walimu Wakuu wa Shule za msingi na sekondari Wilaya ya Pangani
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa