Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wafanya ziara ya kimafunzo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
Hayo yamefanyi
ka leo Julai 26,2024 ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mhe Akida Bahorera amebainisha lengo kuu la ziara hiyo ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ni kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato, hususani katika zao la Mkonge ambalo huzalishwa kwa wingi Wilayani Pangani.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Mkurugenzi Mtendaji Adv Goodlack Mwangomango amepongeza jitihada hizo za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kuja kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya ukusanyaji wa Mapato na kuwaomba watumishi hao kuwa na zoezi endelevu la kujifunza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mhe Akida Bahorera amesema kuwa wamejifunza mambo mengi mazuri ambayo hapo awali walikuwa hawayafahamu hivyo kwa namna moja au nyingine yatabadilisha utendaji wao wa kazi na kuleta matokeo chanya katika Halmashauri yao.
“Tumejifunza mambo mengi ambayo tulikuwa hatuyafahamu hapo awali. Tumejifunza mbinu za ukusanyaji wa mapato zaidi katika zao la mkonge ambalo ni zao tunalolima sana katika Wilaya yetu". Tutaendelea kuisimamia Halmashauri yetu vizuri ".Alibainisha.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Charles Edward Fussi ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kuipokea timu ya wataalam na Waheshimiwa Madiwani, kwani jambo hili linaendelea kuleta manufaa chanya katika ukuzaji wa mapato ndani ya Halmashauri.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa