Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Pangani ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani ambae ni Waziri wa Maji mhe Juma Aweso ,imekagua miradi ya Maendeleo lengo likiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ziara hiyo ilioanza tarehe 21 Novemba 2023, yenye lengo la kutembelea kata zilizopo katika Wilaya ya Pangani na kukutana na Wananchi ili kutatua kero mbalimbali.
Hata hivyo ziara hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani mhe Abdulaman Bonge.
Miradi iliyopata nafasi ya kukaguliwa ni Sekta ya Afya, Elimu pamoja na miundombinu ya barabara ikihusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tanga Pangani Saadani Bagamoyo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa