Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigela alihitimisha ziara ya siku 2 wilayani kuanzia tarehe 19/10/2018 hadi tarehe 21/10/2018, kwa kutembelea Kata 7 kati ya 14 ndani ya Wilaya. Kata hizo ni Mkalamo, Mkwaja, Kipumbwi, Mikinguni, Mwera, Pangani Mashariki na Pangani Magharibi; akiwa ametumia muda mwingi kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao.Ziara hiyo ilikamilika kwa RC Shigela akiwa amegusa sekta zote kwa undani na kutoa dira ya Serikali.
Ziara hiyo RC Shigela aliambatana na DC Pangani Mh.Zainab Abdallah, Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Pangani Mh.Jumaa Aweso ambae alitumia wasaa huo kuzungumza na wapiga kura wake akianza kwa kuchangia ujenzi wa kumbi za Ibada yaani Miskiti na Makanisa ndani ya kata ya Mikinguni, zaidi kwa hisia kali Mbunge alinena mazito kwa kutoridhishwa na mchango wa mwekezaji wa Mashamba ya mkonge ya Amboni kwa jamii na mwisho kutoa kilio chake kikubwa cha Barabara na kuomba ikiwezekana Mh.Raisi akija kwenye maadahimisho ya kilele cha Mwenge mkoa wa Tanga mwezi ujao tarehe 14/10/2018 apite barabara ya Pangani ili kujionea hali halisi ya Barabara hiyo.
RC Shigela alileta tumaini kubwa kwa majibu chanya ya mipango ya serikali juu ya hatma ya Barabara hyoi na kuahidi kuwa barabara hiyo mwezi ujao tenda itatangazwa na ndani ya miezi miwili ujenzi utaanza kwa barabara ya Tanga-Pangani; pia ameahidi kutimiza ombi la mbunge kumuomba Mh.Raisi kupita Pangani kwenye kilele cha Mwenge 14 Oktoba 2018
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa