Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani chini ya DC Zainab Abdallah wamefanikiwa kukutana na kufanya kikao na Mkuu wa Hifadhi ya SAADANI Mama Angella Nyaki. Ufanikishaji huu umekuwa sehemu na mpango mkakati mzito wa kuhakikisha serikali inafanya kazi bega kwa bega na Hifadhi hii kwa manufaa ya pande zote mbili, ikiwa ni Hifadhi ya SAADANI na Wilaya ya Pangani.
Ni wazi Hifadhi hii ipo sehemu ya Pangani kwa upande mmoja na huu ni urithi na Fahari yetu, ni wajibu wetu kuwekeza nguvu, ubunifu, bidii, na kila liwezekanalo kuifanya kua imara, na kivutio chenye upekee kwa taifa letu na kuendelea kuwa na tija katika sekta ya Utalii nchini
Lengo letu kama Serikali ni kushiriki kuitangaza Sekta ya Utalii katika mkoa wetu wa Tanga hususani Wilaya ya Pangani ambayo imebarikiwa kua na vivutio vingi.
Ikumbukwe Hifadhi hii ya SAADANI ni ya kwanza Afrika na ya pili duniani inayopakana na bahari; ikiongozwa na ya kwanza toka taifa la Indonesia.Tunaenda kufungua milango zaidi ya utalii kwa Wilaya hii yenye fukwe nzuri sana za kuvutia,simba na swala wakicheza fukwe za bahari, mto Pangani uliokutana na Bahari ya Hindi, kilimo cha popoo eneo la mauya ikiwa ni wIlaya pekee nchini inayozalisha, kaburi la Abushiri, Lango la kuwapokea watumwa kuingia Pangani, ofisi ya nguli wa fasihi Marehenu Shabaan Robert, kilimo cha mkonge ambapo wilaya hii inaongoza kwa nchi yetu, majengo ya kale, vyakula vya asili na zaidi mazingira ya kuvutia na urithi wa asili ya maisha ya watu wake.
Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Pangani amekubaliana na uongozi wa Hifadhi ya SAADANI kwa yote yaliozungumzwa na kujiwekea mipango na malengo.!
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa