RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ameitaka Taasisi ya Sayansi za Bahari wilayani Pangani Mkoani Tanga iliyopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuhakikisha wanawekeza zaidi kwenye utafiti ili waweze kupata maendeleo makubwa
Dkt Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Sayansi za Bahari kituo cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga tarehe 30/03/2019
.
Na kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah alisema uwepo wa chuo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kitakuwa kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Mh.DC Pangani amesema kuwa kwa sasa bado changamoto kubwa vijana na wananchi wa Pangani hawajanufaika na chuo hicho ambao wanategemea uwezekaji kwenye sekta
ya uvuvi hivyo kuomba chuo hicho kuona namna ya kushirikiana na kuliona hilo na kujipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi na kuwahusisha moja kwa moja wana Pangani kupata maarifa.
Taarifa njema ni kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amelipokea na kulikubali na kusema wanajipanga kulianza mara moja na watajadili namna ya uendeshaji na ujenzi wa kuongeza miundombinu utaanza pia uandaaji wa mitaala ya namna hiyo kuwekwa tayari.Hii ni faraja kubwa sana kwa wakazi wa Pangani na ni picha halisi kuwa ujio wa Chancellor Dk.Jakaya M.Kikwete umeacha alama Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa