SEKTA YA KILIMO
80% ya wakazi wa Wilaya ya Pangani ni wakulima .
HALI YA UPATIKANAJI WA MVUA
Katika maeneo mengi ya Wilaya ya Pangani kumekuwa na hali ya ukosefu wa mvua ya kutosha hususani katika kipindi cha msimu wa masika na vuli la mwaka jana, hivyo kusababisha uzalishaji wa mazao kuwa chini ya matarajio. Takwimu za mvua iliyoripotiwa katika kituo cha Pangani kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita ni kama invyonekana kwenye jedwali :
Hali ya upatikanaji wa mvua kwa kipindi cha mitatau
MWEZI |
KIWANGO CHA MVUA KILICHONYESHA KWENYE MSIMU WA MASIKA NA VULI MWAKA 2014 – 2016 (mm)
|
MSIMU WA KILIMO
|
||
2014
|
2015
|
2016
|
|
|
MACHI
|
124.7
|
196.4
|
22.7
|
MASIKA
|
APRILI
|
116.3
|
137.6
|
368.6
|
|
MEI
|
281.5
|
370.5
|
87.3
|
|
JUNI
|
48.9
|
15.2
|
73.5
|
|
OKTOBA
|
34.6
|
35.7
|
41.8
|
VULI
|
NOVEMBA
|
170.7
|
270.6
|
131.1
|
|
DESEMBA
|
105.1
|
70.5
|
20
|
|
JUMLA
|
881.8
|
1096.5
|
745
|
|
HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA
Wilaya ya Pangani ina jumla ya kaya 14,513 zenye jumla ya wakazi 59502; Mahitaji ya Chakula kwa Wilaya ni Tani 13929 kwa mwaka. Msimu wa masika mwaka huu 2015/16 kuna mavuno pungufu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha kupata mvua kidogo katika kata zote. Mazao ya chakula yanayolimwa ni Mahindi, Mpunga, Kunde, Ndizi, Muhugo na Viazi vitamu. Malengo ilikuwa kuvuna Tani 34,492 lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa tumeweza kuvuna Tani 8,913 za mazao ya chakula, hivyo kuna upungufu wa Tani 5,016 ukilinganisha na mahitaji halisi ya sasa ambayo ni Tani 13,929
Takwimu za uzalishaji wa mazao ya chakula kuanzia 2012 hadi 2016 ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini.
Jedwali Na 05: Uzalishaji Mazao ya Chakula
ZAO |
2012
|
2013
|
2014
|
2015
|
2016
|
|||||
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Mavuno Tani
|
|
Mahindi
|
6590
|
5292
|
6924
|
11983
|
6935
|
12,778
|
7062
|
14124
|
8410
|
84
|
Mpunga
|
-
|
-
|
54
|
38
|
64
|
49
|
194
|
95
|
245
|
0
|
Muhogo
|
2235
|
3278
|
1197
|
5985
|
1290
|
14391
|
135
|
146
|
1724
|
8,792
|
Viazi vitamu
|
47
|
103
|
43
|
148
|
73
|
601
|
1513
|
16643
|
95
|
0
|
Ndizi
|
82
|
62
|
86
|
430
|
137
|
1213
|
151
|
1359
|
129
|
27
|
Mikunde
|
90
|
31
|
96
|
186
|
158
|
121
|
75
|
600
|
204
|
10
|
Jumla
|
9,062
|
8,781
|
8,446
|
18,814
|
8,667
|
29,159
|
9130
|
32,967
|
10,807
|
8,913
|
MAZAO YA BIASHARA
Mazao ya Biashara yanayolimwa Wilayani Pangani ni Mkonge, Korosho, Minazi, Michungwa, Miembe na Ufuta.
Takwimu za uzalishaji wa mazao ya biashara toka Mwaka 2013 hadi 2016 ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini;
uzalishaji wa mazao ya biashara kwa mwaka 2013 hadi 2016
ZAO |
2013
|
2014
|
2015
|
2016
|
||||
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Tani
|
Hekta
|
Mavuno Tani
|
|
Nazi
|
407
|
425
|
10473
|
26498
|
11890
|
29725
|
11132
|
8,150
|
Korosho
|
364
|
65
|
3989
|
689
|
4624
|
524
|
5079
|
630
|
Machungwa
|
312
|
5616
|
847
|
1365
|
1004
|
15060
|
1189
|
15,457
|
Ufuta
|
441
|
308
|
1247
|
1365
|
2526
|
3031
|
27885
|
334
|
Jumla
|
1524
|
6414
|
16556
|
29917
|
20044
|
48340
|
45285
|
14,887
|
USINDIKAJI WA MAZAO:
Wakulima wamekuwa wanafanya usindikaji wa mazao ya muhogo katika kata ya Madanga, alizeti kata ya Kipumbwi, mafuta ya nazi na makumbi ya nazi kata ya Pangani mashariki lakini kutokana na uzalishaji mdogo , usindikaji kwa kipindi hiki haukuwa mkubwa.
MAFANIKIO YA SEKTA YA KILIMO
Wakulima wa korosho Kijiji cha Sange wamenunuliwa mashine za ubanguaji korosho.
Vikundi 7 vya uzalishaji miche ya korosho vimeanzishwa na hadi 2016/17 jumla ya miche bora ya Mikorosho 120,000 na itagawiwa bure kwa wakulima.
• Ushirika wa wakulima wa nazi wamenunua mashine za kuchakata makumbi ya nazi hivyo kuongeza thamani ya zao la minazi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa