Monday 14th, October 2024
@Mwera,Madanga na Pangani mjini
Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Pangani sambamba na ofisi ya mbunge inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wazee wa taifa letu.Tumeamua kuwagusa wazee kwa namna ya tofauti kabisa.na kuja na kampeni maalumu kabisa katika kuazimisha siku ya wazee duniani inayoitwa "NASHUKURU MZEE"
Mambo muhimu yatakayofanyika kwenye kampeni hiyo
.. 1. Neno la kuwashukuru kwa kazi nzito waliofanya hadi sasa kuijenga Pangani na taifa letu kwa ujumla.
.2. Kuwapa zawadi ya uhakika kunako sekta ya Afya kama jambo muhimu zaidi kwao nyakati hizi ikiwa ni kuhakikisha wazee wote ndani ya siku 3 wanapata vitambulisho vyao vya matibabu bure kama ilivyo elekeza serikali ya awamu ya tano.
4. Matibabu,upasuaji vipimo na matibabu bure maalum toka kwa wataalam ndani na nje ya Pangani kwa wiki hii hadi kilele.
5.Vipimo vya macho na wataopatikana na tatizo kupatiwa miwani.
6.Zoezi la uchangiaji damu.
Sambamba na zawadi hii ya kiAfya kwao....! Pia tumedhamiria....!
.
7.Kuwajengea uwezo na kuwapa tumaini jipya na mikakati ya serikali juu yao ikiwemo kujua kero na changamoto zao kutafutiwa ufumbuzi.
8.Mwisho kupata nao chakula cha mchana Nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya na Mgeni Rasmi atakuwa Mh Jumaa Aweso (Mb) - Naibu Waziri wa Maji; atakutakana na kujumuika nao.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa