JINSI YA KUJISAJILI
Ili kupata fursa ya kunufaika na huduma/mradi huu Vitu muhimu ambavyo utaulizwa/vinavyohitajika katika huduma hii ni
Umri
Jinsia
Mkoa na
Wilaya.
HATUA ZA KUJIUNGA
1.Andika neno SAJILI kwenda 15070.
2.Utapokea ujumbe wa kukukaribishwa na kukutaka uchague lugha ili uweze kuendelea (A)Kiingereza (B) Kiswahili. Utatuma herufi ya lugha rafiki kwako.
3.Kisha utatumiwa sms ukitakiwa kutaja umri wako,utatuma umri wako kwa tarakimu. Mfano (18)
4.Utatumiwa tena sms ikikutaka utaje jinsia aidha mvulana au msichana. Utatuma kwa kifupi aidha neno ME au KE
5.Kisha utatakiwa utaje mkoa unaotokea Mfano TANGA na
6.Mwisho utatakiwa utaje Wilaya unayotokea Mfano PANGANI
7.Baadaye utatumiwa ujumbe wa kukujulisha kuwa umesajiliwa “Tayari umejiunga na U-Report.”
Ukiisha jisajili kila wiki utaendelea kupata ujumbe wa kuhitaji maoni yako ambayo yatayafanyiwa kazi na mrejesho utatolewa kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.
Zingatio
Vijana wawe huru kuchangia kwa kufuata maadili na pia katika kujiunga hakutakuwa na utambulisho wako wa jina wala namba yako ya simu.
Huduma hii ni BURE, hautatozwa pesa yoyote kwenye salio lako,kuanzia kwenye kujiunga mpaka kwenye kushiriki kwenye utoaji wa maoni.
Kama Kijana au mdau wa maendeleo ya vijana unaombwa ujiunge na utumie fursa hii kwa maendeleo chanya ya sasa na baadae.
“Wajulishe rafiki zako kuhusu U-Report na jinsi ya kujiunga. Kumbuka SMS zote ni BURE”
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa