Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdallah jana tar 27 Aug.2018 amevuna matunda ya jitihada na maono aliyo pigania; ambapo Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga - Ndugu Percival Salama aliyapokea na kuyafanyia kazi kwa ukaribu sana na leo kupata baraka za viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wataalam wa Halmashauri pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali. .
Kwa mujibu wa historia, Bandari ya Pangani ndio Bandari ya kwanza Afrika Mashariki iliyoanzishwa kabla ya karne ya 6 B.C!!
Mkoa wa Tanga una bandari 2 tu kwa sasa; ambazo ni bandari ya Tanga na bandari ya Pangani. Mamlaka ya Bandari wamefanya upembuzi yakinifu na kugundua tuna bandari 44 zisizo rasmi ndani ya Mkoa wa Tanga; na kati ya hizo 20 zipo Tanga mjini,15 pangani, 12 Mkinga na 1 ipo Muheza. Kamati maalum ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya Mh Shigela (Mkuu wa Mkoa) imefanya maamuzi ya kurasimisha bandari 4 kwa sasa; ambazo kati ya hizi 1 ni Manza Bay (Mkinga), 1 ipo Kigombe (Muheza) na 2 zipo Kipumbwi na Mkwaja (Pangani).
Hatua hii itaambatana na kuirekebisha Bandari ya Pangani mjini; lengo ikiwa ni kuimarisha sekta hii ambayo ni kitovu cha uchumi kwa taifa letu na mataifa makubwa yalioendelea duniani. Mkakati ni kuhakikisha inapofika mwisho wa mwaka huu Bandari hizo 4 ziwe zimerasimishwa.
Hii ni habari njema sana kwa wana Pangani ambapo itafungua milango zaidi ya maendeleo, itaongeza mapato, itawawezesha wana Pangani kupata bidhaa kwa bei nafuu na urahisi; itasaidia katika dhana ya ulinzi na usalama na kubwa zaidi kuifanya wilaya hii kua kitovu cha Biashara na Viwanda.
.Hatua hii ni mwendelezo wa ujenzi wa Pangani Mpya katika kutimiza azma ya maendeleo na mabadiliko ya kweli kila sekta na kwa kila namna kufanikisha malengo na azma ya Serikali ya awamu ya 5; na dhana ya Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Ndugu John Pombe Magufuli
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa