BARAZA LA MADIWANI KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA JULAI _SEPTEMBA, 2024 LA JADILI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO.
Mkutano wa Baraza la Madiwani umefanyika leo Oktoba 31,2024 katika Ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Akida Bahorera.
Aidha mkutano huo ume hudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya, Katibu Tawala Wilaya bi Ester Gama, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Tarafa, Watumishi Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi wa Pangani.
Katika Mkutano huo masuala mbalimbali ya Maendeleo yalipata nafasi ya kujadiliwa ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Mapato na Matumizi na Miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Hata hivyo taarifa zote zilizowasilishwa zilipokelewa.
Kamati zilizowasilisha taarifa ni pamoja na kamati ya Fedha,Mipango na Uongozi, Kamati ya Elimu na Afya, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa