BARAZA LA MADIWANI LAJADIRI TAARIFA ZA UTEKELEZAJI KATA KWA KATA.
Baraza la waheshimiwa Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Aprili 29, 2025 limeketi na kujadiri taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizopo katika kata zote 14 za Wilaya hiyo, kwa kipindi cha robo ya tatu kuanzia mwezi januari hadi machi 2024/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya zamani.
Kikao hicho kimeongozwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri mhe Zainabu Mvaa ambapo alisisitiza kuwa changamoto zilizowasilishwa zifanyiwe kazi kwa wakati ili kuendelea kuiletea maendeleo Halmashauri yetu.
Aidha katika kikao hicho Waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kuchangia mada kwa nyakati tofauti na wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo na changamoto zake pamoja na utatuzi wake.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa