Baraza la Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Pangani limepitisha mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kukusanya na kutumia shilingi bilioni 23, 963,702,805.00 kutoka vyanzo vya ndani, ruzuku kutoka Serikali Kuu, Miradi ya maendeleo na Mishahara
Mpango na bajeti huo umepitishwa katika kikao maalum cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani kilichofanyika leo tarehe 05 Machi 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya zamani ambapo kimehudhuriwa pia na Kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wananchi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa