BARAZA LA WAFANYAKAZI PANGANI LAJADILI RASIMU YA MPANGO NA BAJETI 2024/2025
Baraza la wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani limejadili mapendekezo ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuandaa bajeti inayotekelezeka.
Kikao hicho cha kujadili rasimu ya bajeti hiyo kimefanyika leo Februari 21, 2024, katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Kikao hicho pia kimejadili utekeleaji wa bajeti inayoelekea ukingoni kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo wajumbe wa baraza hilo wameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kupitia bajeti yake.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani , Juma Mbwela amewahimiza watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa uadilifu.
Kwa upande wake Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Simeon Vedastus amesema kuwa Hadi kufikia 31 Disemba, 2023, jumla ya Tshs. 9,990,197,202.00 sawa na 52% ya Tshs 19,189,201,000.00 zimekusanywa kutoka
vyanzo mbalimbali vya mapato.
Baraza limepokea na kupitisha Rasimu ya mpango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inaomba kuidhinishiwakukusanya na kutumia mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani kiasi cha shilingi 19,552,457,000.00 ikiwa ni ongezeko la takriban 2% ya bajeti ya mwaka 2023/2024.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa