Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah, amefanya ziara na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Ziara hiyo imefanyika Jumatatu Oktoba 30,2023, katika kata ya Mwera ambapo amekagua ujenzi wa darasa shikizi Stahabu na kufanya mkutano na wananchi.
"Niendelee kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya dkt Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuiwezesha Wilaya ya Pangani kupata fedha za miradi ya maendeleo,lakini pia mbunge wetu wa jimbo la Pangani mhe Jumaa Aweso kwa kuwa mstari wa mbele kuisemea Wilaya yetu".
Mhe Zainab amewataka wananchi wa kijiji cha Mikinguni kuendelea kushikamana na kushiriki miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mikinguni mhe Yoel ameishukuru ziara hii kwani imeendelea kufungua fursa na kutatua changamoto zinazopatikana katika maeneo yao.
#panganimpya
#hakunakilichosimama
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa