Pangani, Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mheshimiwa MUSSA KILAKALA ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya hiyo.
Kikao hiko kilichokuwa na lengo la kujadili na kutoa maoni katika dira ya Taifa 2025 - 2050, kimefanyika leo Jumatatu 29 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Wajumbe kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa walijadili kwa kina na kutoa maoni juu ya uelekeo wa Taifa la Tanzania kwa miaka 25 ijayo katika nyanja zote zikiwemo afya, elimu, michezo, miundombinu, kijamii, kisiasa,na kiuchumi
Kikao hiko kilihudhuliwa na makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, vijana, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi na asasi mbalimbali.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa