Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Gift Isaya Msuya leo Aprili 28, 2025 ameongoza kikao cha kamati ya Afya ya Msingi ( PHC), ukumbi wa Halmashauri kwaajili ya kujadili mikakati ya zoezi la kitaifa la utoaji wa dozi ya nyongeza ya chanjo ya sindano ya Polio _IPV2. Inayotarajiwa kuanza mwezi wa tano.
Mhe Gift amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wote ili waweze kujikinga na ugonjwa huo ambao ni hatari sana kwa maisha ya watoto wetu.
Aidha amesisitiza kuwa nyongeza ya dozi la pili ya chanjo ya polio ni hatua muhimu katika kuimarisha kinga kwa watoto dhidi ya ugonjwa hatari wa polio.
Ikumbukwe kuwa chanjo ya Polio hutolewa kwa watoto mara tu wanapozaliwa na kuendelea kutolewa wanapofikisha umri wa wiki 6, 10 na 14.
Katika kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa wa polio nchini, watoto wote wataanza kupatiwa dozi ya pili ya chanjo ya Polio IPV2
Wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana kuimarisha uhamasishaji wa zoezi hilo ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa huduma hiyo muhimu
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa